Mariam's Story
This story and photography is part of the exhibition Ethical Storytelling: Feelings and Memories.
#EthicalStorytellingExhibit
​
Untitled Story - Mariam
Kulikuwa na Kijiji kimoja kilichokuwa karibu na baharini kiitwacho kanamai. Katika Kijiji hicho paliondokea mama mmoja aliyefiliwa na mumewe. Mama huyo mjane alijaaliwa na watoto watano. Wasichana watatu na vijana wawili. Wasichana hao kwa majina walikuwa Saida, Saada na Zubeda. Vijana walikuwa Sudi na Zakariah. Maisha ya huyo mama yalikuwa magumu sana baada ya kifo cha mumewe.
Mama huyo alikuwa mwenye huzuni na mawazo mengi moyoni. Kwa jinsi alivokuwa akiishi na mumewe pamoja na watoto wao, maisha yao yalikuwa yenye furaha na bashasha. Mama huyo alimzoea sana mumewe, walikuwa wakishirikiana na pia kusaidiana kwa kila mambo. Marehemu mumewe alikuwa mtu mwenye furaha kila wakati,pia alikuwa akipenda Kila mtu .Kazi yake ilikua ya udereva. Akiwahi kibarua hicho yuafanya akikosa anashukuru na wanasaudiana na mkewe kazi za nyumbani. Mkewe alikuwa akifanya biashara ya kupika vyakula. Mumewe akipata kibarua, mshahara wake japo kidogo anchanganya na mkewe wanapanga mambo yao vizuri kwa kidogo walichopata.
Pesa aliyokuwa akipata baada ya kufiliwa na mumewe hazikuweza kutimiza mahitaji yake na wanawe. Alikuwa amezoea kuchanganya kidogo apatacho na mumewe, kilichoweza kukidhi mahitaji yao bila wasiwasi. Kama wahenga walivyosema haba na haba hujaza kibaba.
Mama huyo akawa kila siku anapomaliza biashara yake akihesabu pesa zake huwa anamkumbuka mumewe. Siku moja akatembelewa na rafiki yake wa karibu aitwae Salma. Salma alimwambia, "Rafiki yangu kwa hali hii ngumu ya maisha unayopitia, je ungependa kusafiri ukafanye kazi ya nyumbani nchi ughaibuni?" Mama huyo alikubali na kusema akipata ajenti mzuri wa kusafirusha watu basi hana budi kukataa.
Salma alimwambia kuna ajenti wanakuja huku Kijijini kutafuta watu wanaotaka kusafiri, na alikuwa na nambari ya simu ya ajenti hivyo basi atampigia waonane. Mama huyo alisema sawa. Siku moja akaja yule ajenti wakazungumza na yule mama. Wakajitambulisha, ajenti huyo aliitwa Mwinyi Bakari. Ajenti hyo alikuwa na ofisi yake mjini Mombasa, alimuelekeza huyo mama katika ofisi yake ili wakaelewane na apate kusafirishwa.
Mama huyo alifurahia na kurauka asubui kufanya biashara yake Kisha kwenda katika ofisi ya huyo ajenti. Kwa bahati mbaya hakuwa anajua lolote kuhusu usafiri wa kwenda ughaibuni. Alipofika kwa ajenti alikaribishwa vizuri. Baada ya mazungumzo marefu ajenti huyo alimwambia kuwa kazi atakayofanya ni ya uyaya nchini Saudia Arabia mkoa wa Riyadh. Kazi hiyo ilikuwa ya kuangalia mtoto mmoja. Mama huyo alikubali na aliona ni kazi nzuri yenye amezoea kulea wanawe. Aliambiwa mshahara ni elfu thelathini na contract ya miaka miwili. Alikubali na akatozwa elfu kumi na saba , kuenda kupimwa ajue Hali yake Kisha ndo asafiri. Pesa hizo mama huyo alienda kukopa kwa rafikiye Salma na kuahidi kurudisha atakaposafiri. Salma alimkopesha, mama huyo alipeleka hizo pesa kwa ajenti na kungoja safari. Alienda medical Nairobi na alikuwa mwenye afya nzuri hivyo bas akaambiwa atapewa tikiti ya ndege baada siku kadhaa.
Baada ya wiki moja ajenti alimpigia simu na kuambiwa tikiti yake ipo tayari na atsafiri baada ya siku tatu. Mama huyo alienda kwa mama yake mzazi na kumueleza kuhusu safari yake na kumuomba abaki na wajukuu zake mpako atakaporudi panapo majaaliwa. Mama huyo alimshukuru sana mamake kwa kumkubalia maombi yake, alitafuta dada wa kazi ili amsaidie kazi pamoja na watoto wake.
Baada ya siku tatu mama huyo alikuwa tayari kwa safari akarudi ofisini kwa ajenti huyo. Mama huyo alipewa karatasi atie saini. Ajenti alimwambia hiyo karatasi ni ya contract ya kazi yake, siku atakazo kwenda kufanya Kazi pamoja na maelezo ya mshahara wako. Mama huyo alisaini na kupelekwa airport.
Alibahatika kusafiri akafika salama salmini. Alipofika uwanja wa ndege wa Saudia Arabia mida ya saa mbili asubui alipokonywa passpoti yake Kisha akapelekwa ndani ya chumba kilichokuwa na wafanyikazi wengine. Alifungiwa humo akaambiwa asubiri tajiri yake mpaka atakapokuja kumchukua.
Alishinda apo bila ya kupewa chakula chochote. Tajiri yake alikuja kumchukua saa moja ya usiku, wakasalimiana na kuenda nyumbani kwake. Alipofika nyumbani alikaribishwa Kisha akaambiwa afungue bagi lake. Tajiri huyo alilichakura bagi la huyo mama. Kisha akamwambia kuwa hatazivaa nguo zote alizokuja nazo na hawazitaki watazitupa zote. Akapewa nguo mbili Kisha akapokonywa simu yake. Akaelezwa kuwa amekuja kufanya kazi kwahiyo simu hairuhusiwi. Aliahidiwa kurudishiwa simu yake endapo atamaliza contract yake, akaelezwa kuwa atakuwa anatumia simu ya tajiri yake mara moja kila mwisho wa mwezi.
Mama huyo aliulizwa kama anajuwa alikuja kufanya kazi gani? Mama huyo alijibu ndio, kazi ya uyaya. Akaambiwa mi ukweli lakini sio mtoto mmoja ni watoto sita. Pia sio kazi moja tu ya watoto bali pia kazi ya nyumbani zote katika kasri hilo ikiwemo kusafisha, kupika, kufua, kupiga pasi na pia atafanya kazi za huyo tajiri kuanzia saa kumi na moja asubui mpaka saa kumi jioni. Kama umemaliza ama hujamaliza nitakupeleka nyumbani kwa mamangu ukamsaidie kazi za nyumbani.Sababu mfanyikazi ni mmoja na nyumba ni kubwa sana.Mama huyo alishituka sana kusikia kazi hizo zote nizake.Kisha tajiri aka muliza jee unajuwa mshahara wako ni pesa ngapi.Mama akajubu,"najua nishilingi elfu thelathini". Tajiri akamjibu la mshahara wako ni elfu kumi na nne.
Mama huyo alizidi kupigwa na butwa na akashindwa afanye mini.Akaomba simu ili azungumze na ajent wake kuhusu aliyomwambia na yalikuwa siyo.Tajiri alikataa kumpa simu akamwambia,ushafika na utaanza Kazi sasa hivi.Mama huyo nakuchoka kwake kwa safari na njaa aliokuwa nayo kutoka asubuhi hadi usiku.Alifanya Kazi kishingo upande hakujua amueleze nani shida zake.Hapo ndipo aligundua ya kwamba yule tajiri alimdanganya.
Mama alianza kazi usiku saa mbili akimaliza ni mwendo wa saa sita za usiku.Akaonyeshwa mahali pakulala akashtuka sana.Kwani aliambiwa alale chini na akapewa blanketi moja.Hajui alitandike chini ama ajifinikie Mama huyo alitandika blanketi chini nusu akalalia na nusu akajifinikia.Kwasababu kulikuwa na baridi nyingi sana.Alilala na njaa hakupewa chakula chochote.Asubuhi kulipo kucha akaanza kazi zake kama alivyoelezwa.Ilipofika saa kumi jioni,alipekwa kwa mamake yule tajiri akafanye kazi hadi saa saba za usiku ndio akarudi nyumbani kulala.Huo ndio ukawa mtindo wa wake wa wakufanya Kazi kila siku.
Baada ya miezi mitatu mama huyo aliuguwa sana.Akamuomba tajiri wake ampeleke hospitalini, tajiri alikataa akamnunulia dawa za maumivu akampatia . Alijikaza kisabuni lakini ya siku kadhaa alizidiwa akashindwa kufanya kazi. Mama alimuomba tajiri wake kama hawezi kumtibu amrudishe kwao. Tajiri akamjibu afanye kazi miezi mitatu bila malipo mwisho aweze kumkatia tikiti ya kurudi kwao.Mama huyo alijuta majuto ya firauni.Akaseme ni sawa tu.Alijikaza na ugonjwa wake akafanya kazi na huzuni nyingi sana moyoni.
Baada ya miezi mitatu alikatiwa tikiti akarudi kwa bila mafanikio yoyote.Alipofika kwao familia yake ilishituka sana kumuona amekonda sana .Kabla haja safari alikuwa ni mama amenona kiasi napia ana afya nzuri sana.Alikuwa amedhohofika sana kwa Kazi nyingi pia kukosa kula vizuri na kulala kwa masaa machache.Familia yake ilisikitika sana pia walishukuru sana kwa kurudi salama.Wamlichukua na kumpeleke hospitalini.Alitibiwa akapigwa picha akaonekana mapafu yake yalikuwa yameingia maji kwa baridi nyingi pia kwa kulala chini,pia akapatikana na shida ya mgongo na kiuno na pia alikuwa ana maumivu ya miguu kwasababu ya kusimama muda mrefu kufanya Kazi bila mapumziko.Aliruhusiwa kurudi nyumbani na akapewa dawa za kutumia.
Baada ya wiki mbili rafiki yake Salma alipata habari rafiki yake amerudi. Alishangaa sana akenda kumuona.Rafiki yake alimsimulia kisa kilicho mpata akahuzunika sana.Salma alimpa Pole sana pia alimshauri ampelke katika ofisi ya shirika la"HAAT KENYA".Rafiki yake akamuliza shirika hilo linahusika na Kazi gani? Akamjibu linafanya awareness of human trafficking.Pia hapo wanafanyia watu counseling.Rafiki yake alikubali kwenda katika shiriki hilo.
Alipofika huko alihudumiwa vizuri sana.Alifanyiwa counseling kisha akapewa msaada ili ajiendeleze na maisha yake.Mama huyo alishukuru sana shirika hilo la HAART KENYA kwa maidha yao na usaidizi wao.Kwani alikuwa ameona maisha yake yamefika mwisho.Kwa sasa mama huyo yuko vizuri na watoto wake napia anajiendeleza vizuri na maisha yake".
​

