Msichana Wa Kighetto's Story

This story and photography is part of the exhibition Ethical Storytelling: Feelings and Memories.

#EthicalStorytellingExhibit

thumbnail_Janet-2.jpg

Untitled Story - Msichana Wa Kighetto

 Sijui nianzie wapi, nimalizie wapi.

Majina Yangu naitwa Janet Wambue, mimi ni mzaliwa Murang’a. Mimi kwangu naeza sema nimepitia mangumu kwa hii maisha, juu kutoka kuzaliwa, kuwa mkubwa, hapo nime fikisha tunaweza sema tuu ni Mungu. Nilizaliwa katika kijiji kimoja huko Murang’a chaitwa Kabati. Na nilizaliwa na wazazi wangu wawili na wote wako, na hapo ndiyo nilijua shida ndiyo kusema nini.

Babangu na mamangu walikuwa wazazi wanao pigana sana, walikuwa wana pigana na mimi niko hapo, najionea kila kitu walikuwa wana fanya. Ilifika mahali mpaka kwenda shule ikawa shida. Juu babangu kumuelewa ilikuwa shida juu yeye alikuwa mlevi, anavuta mpaka bhangi. Na pia alikuwa muuzaji wa banghi, na mwishowe alishikwa na polisi, tuka baki na mamangu, na ndugu zangu wadogo, na ukumbuke mimi ni first born kwetu.

Mamangu aliwachwa na hii biashara ya baba yangu na pia yeye akashikwa na akafungwa. Baadaye, guka mwenye amemzaa babangu alipojua sasa babangu afungwa ndani, akakuja na watu wengina kwa boma yetu, akasema hiyo shamba yote ameiuuza. Sasa vile guka yangu alisema shamba imeuzwa na tuka pewa 24 hours notice tuwe tumetoka kwa hiyo shamba. Shosho yangu aliposkia alikuwa mgonjwa na mama yangu naye ni kama wazimu juu alikuwa na mtoto mdogo pia. Ilibidi tuka toka kwa hiyo shamba, mama yangu aka komboa nyumba Kabati tukaanza kuishi huko, mimi, ndugu zangu, mama yangu na shosho yangu.

Venye tuliendelea kuishi huko maisha ikawa ngumu nika ona hatuwezani, mama yangu kwenda kibarua hawezi juu ako na mtoto mdogo ana nyonyesha. Na mimi naenda shule, na hao wengine pia ni wadogo. Dakika ya mwisho nilishindwa kuendelea na masomo.Nilipo shindwa kuendelea na masomo, nikaanza kwenda vibarua mimi mwenyewe nikiwa msichana mdogo, naenda kuchuna kahawa huko kwetu nyumbani niki enda nikilipwa.

Juu nilikuwa najaribu saa zingine naenda nachuna gorogoro mtaani, nalipwa 90 bob. Nikilipwa napitia kwa soko na buy unga kilo moja na nusu na mboga, naenda nazo nyumbani napelekea mama yangu. Mama yangu ali pokuwa ana niona alikuwa analia sana, juu haku imagine mimi nitakuwa ni kama baba wa hiyo familia.

Siku moja rafiki yangu alikuwa ameenda Nairobi kwa aunty yake, aka kuja nyumbani kutembea. Alivyonikuta kwetu, nikamwambia mi naweza taka twende na yeye Nairobi. Aka niambia ni sawa, siku ili fwata akakuja kwetu aka nichukua, tukaenda na yeye Nairobi. Although hata nikiwa nyumbani nilikuwa natamani kwenda Nairobi, sasa ndiyo nika pata wakati wa kwenda Nairobi.

Nika kuja huku Naitrobi, nikifikiria mahali naletwa nilishutuka sana kuji kuta niko kwa nyumba zingine hata zenye tulikuwa tume komboa ni mzuri hata kuliko zenye mahali nilikuja Nairobi. Nika letwa Mathare, nika anza kuishi Mathare.

Mathare hakuna kazi ingine ninge fanya, so nika andikwa kulabu huko ya kuuza chang’aa. Nika uza, nika uza, nilikuwa nalipwa mia moja per day, na hizo pesa zilikuwa zina nisaidia juu siku hiyo hakukuwa na M-pesa, lakini najaribu juu chini, naenda nyumbani napelekea mama yangu pesa.

Niliendelea hivyo, ndiyo marafiki zangu wenye nilienda nika juana nao huko waka nionyesha biashara ingine. Tukakuwa tunaenda town, wakaniambia tunaenda reggae. Sikukataa, nikawafwata tuka enda nao.

Vile tulienda ile biashara nime semwa mwanzo, ndiyo sasa nika ingililia. Tuka anza kuwa tunaenda kujiuza kilabu igine ina itwa Sabina Joy.Tuki enda huko una pata mwanaume anakuambia anakupea mia mbili, na juu mimi nilikuwa mgeni kwa hiyo biashara hata nikiingia  huko walikuwa wanajua wageni ni akina nani waki ingia.

Mi nilipoingia nikakuta mwanaume wa kwanza aka kuja aka niambia ananitaka, na juu nilikuwa nimeelezewa, nikakuta nimeanza hiyo biashara. Nakumbuka hiyo wakati siku moja ya kwanza nililala na wanaume saba, kila mwanaume ana kupea mia mbili, mwingine ana kupea mia tatu, hivyo hivyo nikaona hiyo siku niko na pesa mingi sana. Siku iliyofwata nikaenda kwa ile club nilikuwa nafanya kazi, wale wale wasichana waka kuja wakaniambia twende nao town, nikawaambia nimechoka, twende kesho. The following day tukarudi hiyo kazi. Venye tulienda nikajikuta nimekuwa addicted na hiyo job. Nilifanya hiyo kazi ya kujiuza, na lazima ungeenda huko ukiwa umejitibu, na kujitibu lazima utumie mihadarati ndiyo uende huko ukiwa uko sawa, kichwa kiko sawa.

Niliendelea hivyo kabisa, so pesa nili kuwa napata, juu nilikuwa najua shida yenye iko kwetu, na baba yangu alikuwa jela ilibidii sasa nasaidie mama yangu, ni kama mimi ndiye bwana ya hiyo familia. Niliji tahidi kabisa kabisa, lakini mama yangu hakuwa ana jua kazi nilikuwa nafanya, mi nilikuwa namwambia tuu nafanya kazi ya nyumba. Nilikuwa napelekea mama yangu pesa, mimi mwenyewe, naenda nampelekea pesa nikiona watoto wetu, hivyo hivyo.

Nikiendelea na hiyo kazi na hii kukaa Mathare nikakutana na kijani mmoja anaitwa Mwas. Mwas alikuwa anaogopwa sana, Mwas huko kulikuwa kwao but yee hakuwa anakaa huko, alikuwa anakaa Buru Buru.

So Mwas siku moja aka alinikujia kwanza na ukali sana, akaniambia nipande juu niende kwa stage. Juu namwogopa na watu pia wana muogopa hakuna mwenye anaweza kuulizia, nikapanda juu kule aliniambia. Nikajikuta niko kwa stage, aka kuja tuka ingia kwa gari, tuka enda mpaka kwake. Vile tuliingia kwake, Mwas kwanza aliniuliza kama nimekula, juu ile kumwogopa nika mwambia ndiyo. Mwas nilikuta ameniletea maziwa ile ya Moks, hakuniekea kwa glass, aka niambia nikunywe.

Nilipokunywa me sikujiskia tena, ni kama  alinitilia dawa. Nililala na asubuhi yake kuaamka, ile naamuka nikakuta ameniwekea nguo zangu kwa karai iko na maji. Nika muuliza kwanini alifanya hivyo? Hakunijibu. Ilipofika kitu saa nne, Mwas aliamka na akatoka na akanifungia nje. Ilipofika kitu saa saba ama saa nane, Mwas aka rudi kwa nyumba, aliporudi, alikuja na chakula aka niambia nikule. Juu nilikuwa naskia njaa juu kutoka hata jioni sikuwa nimekula ili bidi nikule.

Nilipomaliza kula, Mwas akubali nianike hizo manguo haladu niende kesho asubuhi. Asubuhi yake kufika nikakuta tena manguo zangu ni baridi. Nika muuliza “ni nini tena kwani hatukuwa tume ongea?” Mwas hakunijibu. Ilibidi nikae kwa Mwas wiki nzima, kama sijaenda Mathare.

Venye nilirudi Mathare, nikaenda kwa wale marafiki zangu, wakaniuliza “kwani ulienda wapi?” NIkawaambia Mwas alinichota, tuka enda na yeye kwake. Venye niliwaambia nafikiria kurudi kwetu nyumbani badala ya kukaa hii maisha naishi, kulikuwa na dem mmoja alijitoa aka enda akambia Mwas kenye nimesema.

Hata hatukumaliza dakika tano, Mwas akakuja akaniambia masaa ya kutembea imeisha, twende nyumbani. Ilibidii tuu nimfwate juu alikuwa ana ogopwa pia mimi nilikuwa namwogopa. Tena nikafwata Mwas tuka enda na yeye. Vile tulienda kwa Mwas, sasa hakuna hata akanipea onyo “usitoke hapa hata usijaribu kwenda Mathare.” Mi nikaona dakika ya mwisho hata heri nitoke kwa Mwas niende kama nimeenda kwetu nyumbani. Sikuenda.

Nilikaa huko tuu kwake, nilipo kaa, nilipofikisha kitu miezi tatu huko, nika pata nimekuwa mja mzito, niliambia Mwas venye naskia, Mwas hakuamini, akanibeba aka nipeleka Hosi nikapimwa nikaonekana niko mja mzito.

Mwas hakukasirika akaniambia tukae. Tulipokaa, mimba ilipoenda kufika miezi sita ndiyo Mwas hakukuja kwa hao. Nkamgoja hakukuja na the following day Mwas bado hakukuja.

Nilikuwa naskia nimechoka, nika jiuliza niende Mathare nimtafute ama?

Siku ya tatu sasa, nika amka nika enda Mathare. Kwenda mathare naona kila mtu ana nitazama, wana niangalia, hakuna mwenye ana nisemea. Ndiyo nika enda kwa marafiki zangu nika waauliza kwani ni nini? Marafiki zangu waliniambia “Mwangi walienda round na Mwas, waliuliwa.”

Nilishutuka, mpaka nika skia naweza  jifungua hiyo wakati, lakini Mungu alinipea nguvu, dakika ya mwisha nikasema wacha mimi nirudi kwa nyumba, nitakuja kesho.

Ka naenda nyumbani sikujua dadake na brother yake wananifuata, juu hawakuwa wanajua kwenye Mwas anaishi. Vile nilifika kwa nyumba kwa mlango ndiyo hao. Badala hata wanipe pole, walianza kutoa mavitu nje. Nikaona wakatoa mattress, viti, meza, wakatoa kabati, wakatoa kitanda. Wakatoa kila kitu, kwenye walibakisha kwa nyumba ni nguo zangu.

Dakika ya mwisha nika wauliza kwanini wanafanya hivyo? Wakaniambia “nijue vile nitafanya, ni mimi niliuwa brother yao nirudi Mathare.” Nililia sana. Nikabeba manguo zangu masaa ya jioni, nikarudi Mathare, kwenda kukaa kwa ule rafiki wangu.

Venye nilirudi huko, sa ujue sina otherwise, mimi si vile nilikuwa kwanza. Na nikienda Mathare nilikuwa nimeenda nitafute kazi ili nisaidie wazazi wangu. Sasa mimi nika kuwa niko na shida mara dufu. Juu sasa niko mja mzito, nimenyang’anywa kila kitu,nime anchwa bila kitu, so nitafanya nini? So ilibidii tuu nirudi ile job nilikuwa nafanya.

Nika rudia kazi ya kujiuza tena, nikaanza kwenda town nipate pesa, nijilishe mimi na nilishe mwenye nimebeba. Nikaenda, mpaka wakati niliji fungua, na ukumbuke naenda town nikiwa mja mzito. Na hao wanaume bado wanaona venye ume kaa, lakini hawajali na pia mimi sijali juu nataka pesa ya kukula, na ya kujivaa na kutafutia huyo mtoto manguo na nini, so ilikuwa ina bidi tuu naenda.

Nilipo jifungua, nilijifungua mtoto msichana. Nilipojifungua mtoto niliendelea kuishi kwa huyo rafiki yangu. Lakini rafiki yangu alifika mahali aka choka na mimi. Niko na rafiki mwingine aka niambia “Wambo usijali, kuja tukae na wewe.” Nikaenda kwake, nikakaa. Nilikaa almost miezi tatu kwa huyo msichana, nikamwambia nafikiria nianze kuacha mtoto, nimtafutie mama wengine alale naye, mi naenda town.

Ndiyo nilifanya, nikatafuta mama, mama aka kuwa mzuri. Alikuwa mama mzee namwachia mtoto mi naenda town, nakuja asubuhi nachukua mtoto wangu naenda kulala.Juu hakuna kitu ingine nilikuwa nafikiria kwa maisha yangu, ilikuwa tuu kujiuza, kuvuta bangi na kuuza chang’aa, hakuna kitu ingine nilikuwa naeza fanya. Ndiyo ika fika mahali, sasa nikitafuta pesa nika komboa nyumba yangu ya mia saba, nika nunua mattress, nika anza kukaa na mtoto wangu.

Mtoto wangu alipofikisha miezi sita na mama wangu hakuwa ana jua mimi niko na mtoto, juu niliikuwa nime ficha sana, hata nikuwa mja mzito zikuenda nyumbani. Nilikuwa tuu natuma pesa kidogo kidogo tuu, so mama yangu hakuwa anajua shida yenye napitia huko Mathare. So mtoto alivyofika miezi sita nika enda nyumbani. Mama yangu ali shtuka sana venye aliona niko na mtoto lakini nikamwelezea shida niliyopitia mama yangu, haikumshika sana.

Nikamwachia mtoto, aka kubali nikarudi Nairobi. Niliporudi Nairobi si kazi ni ile ile venye nilirudi Mathare. Nikarudia tuu ile kazi yangu ya kwenda town, na pia niko club ingine hapo nauza chang’aa. Nauza chang’aa mchana, jioni naenda town. Hivyo hivyo napata doo natumia mama yangu. Napata pesa natumia mama yangu. Niliendelea na hiyo maisha mbaya kabisa, hapo hapo ndiyo nilikaa almost miakaa kadhaa.

Nikaenda hivi nikakutana na jamaa mwingine pia. Huyo jama aka kuja kwanga, tukaanza kuishi kwangu. Tutakaa, ye anajua kenya nafanyanga lakini hakuwa ana niuliza, although alikuwa anajua ile biashara mi hufanya. Lakini sometimes alikuwa ana niambia nisienda. Saa zile ameenda roundi zake amepata doo ananiambia nisienda, na nilikuwa nakubali kidogo akiniambia nisiende juu ananipea doo kwanza ndiyo nilale nisitoke.

Tukakaa na nikajikuta juu ya mapenzi, nimependa yule kijana, na tena nika pata mimba yake. Kupata mimba yake nikajifungua kijana. Nilipo jifungua kijana, tukakaa na babake mpaka mtoto wangu alipofikisha miaka mbili, pia yeye akauliwa. Vile aliuliwa pia yeye alikuwa mwizi. Yaani kusema ukweli mimi nilikuwa nakaa maisha mbaya. Na ukumbuke, nilikuwa nimelelewa maisha ya shida, nikifikiria mi niende nikuwe mzuri ama niende nipate kazi mzuri nisaidie wazazi wangu sikuweza. Juu imagine msichana wa class 5 angefanya kitu ingine gani? Na venye niliingia ghetto, ghetto hakuna maisha ingine mzuri. Kusema haki na ukweli ghetto siyo mahali hata ya kulelea watoto.

Juu hiyo ndiyo maisha yenye niliingilia, na nika jikuta sasa ni kama nimekuwa addicted na hizo maneno. Vile huyu alizikwa, wazazi wake pia wanataka kuja kuchukua mali yangu, lakini sasa mi nikawaambia hakuna kitu ina weza bebwa juu hizi vitu ni zangu, hakuna kitu brother yenyu alikuwa nayo. Nao watu waka waingilia sana wakawaambia, “enyewe brother yenyu alikuwa amewekwa na Wambo, hata kama wamezaa alikuwa amewekwa. So hakuna kitu yenye mnaweza kubeba huko.” Sister yake mkubwa juu alikuwa anakaa huko Mathare aka kuwa na aibu, dakika ya mwisho mimi nilipeana manguo na viatu, nikapeana mimi mwenyewe kwa kutaka.

So venye tulikaa kaa huyu sister yake mkubwa tuka tengeneza tukakuwa marafiki, so hata nikienda hizo maraundi zangu ni yeye nilikuwa naachia mtoto. Ilifikia mahali hiyo ndiyo kazi yenye najua, hakuna kitu ingine naelewa. Tuakakaa hivyo, nalea huyo kijana siku mpelekea mamangu na ule mwingine ako nyumbani msichana. Although nilikuwa nikipata doo natuma nyumbani, ya huyo msichana pamoja na wale watoto wetu. 

Tukakaa hivyo, ndiyo baba yangu alikuja kaaachiliwa, na akarudi atakaishi kwa ploti juu shamba ilikuwa imeuzwa na baba yake. Baba yangu alianza kushonea watu viatu huko town ya kwetu, na mama yangu ali mkaribisha na akaacha kuuza bangi na akakuwa baba mzuri, hata kupigana vita waliaacha na akanza kukaa nyumbani.

So mi nikakuwa pia venye nazidi kuzeeka nazidi kuwasaidia. Nikipata doo natuma nyumbani, na watoto wetu pia walikuja waka kuwa wakubwa. Mmoja akamaliza form 4, huyo mwingine aka maliza form 4, mi ukumbuke mi nilifika class 5, lakini nikasaidia mama yangu kulea watoto wake na kuwasomesha.

Nawasaidia na nini? Na hii biashara ya kujiuza. Kusema ukweli hakuna kazi ingine nilikuwa nafanya, ni kuuza chang’aa na kuuza mwili yangu, hakuna kitu ingine nilikuwa najua. Nilifika mahali mama mmoja anaitwa mama Diana, alikuwa ana niuzia panties, aka niuliza kama naeza taka anipelekee soko niuzange hizo panties. Nika mwambia, “Aii, si kazi nzito?” Akaniambia siyo nzito, nikamwambia akikuja siku ingine tutaenda na yeye.

Tulipo enda na yeye Gikomba, tuka nunua manguo, nika nunua ya mia tano juu nilikuwa na bahatisha bado. Kukuja aka nisaidia mpaka kuziuza. Zingine tuka kopesha lakini kufika kwa nyumba nilikuwa na elfu moja. Nikaona enyewe hii kazi ni nzuri hata kuliko yenye nilikuwa na fanya, na hii hulali kwa baridi, hakuna mtu anakushika shika, huna aibu yoyote, nikaona heri hata hii kazi.

Nika anza kuuza manguo, hata mi mwenyewe najipeleka juu venye alinifundisha, nikajua places za kwendea manguo. Baada ya masiku, mama mwingine alikuja huko Mathare akasema aliskia kuna vile watu wanapelekwa Saudi Arabia na wanafaulu juu huko watu wanalipwa pesa mingi.

Tulikuwa tunaambiwa ni 30,000 wengine wanasema 24,000, wengine 26,000. So uki fanya hesabu unaona enyewe hata heri uende huko juu huko at least kuna pesa. Huyo mama  alikuja kwangu akaniuliza kaa naeza kubali nika mwambia “eeh.” Akanipeleka town kwa agent wao, nikajaza makaratasi, everything. Baadaye niliambiwa nime faulu, sasa tunaweza enda.

Venye nilipekwa Saudi nilipelekwa place inaitwa Madina. Kwenda kwa hiyo place nilikaribishwa vizuri na mama wa hiyo familia. Tulifika tukiwa wasichana wawili, mmoja muEthiopian na mimi. Sasa huyo MuEthiopian kazi yake ilikuwa ya kupika na kufanya kazi za nyumba, mi nikaambiwa kazi yangu itakuwa ya kuosha mama na kumpea dawa.

Sikuwa najua mama ni mgonjwa, ugonjwa gani, nilikuwa naambiwa ni kumuosha na kumpea dawa, nika sema hiyo kazi ni mzuri. Nilipokwenda kuonyeshwa mama ni mgani, ni mama mzee hivi, alikuwa na vidonda kwa mwili, ni kaa alikuwa na ile ugonjwa ya kisukari, so ilikuwa imemshika vibaya ndiyo maana alikuwa na vidonda kwa mwili.Kazi yangu ilikuwa kumwosha, na jamani wacha nikule shida kwa hiyo familia. Mama namuosha, nikimaliza kumuosha zile maji, ka alikuwa anajua kenye anafanya, ana nimwagia zote kwa uso, hata zingine nakunywa nameza. Na ukumbuke, ziko na ngozi zake, madamu, usaa zote ziko hapo. Na lazima ninge fanya hivyo kila siku. Namuosha, namkausha, nampaka dawa yenye alikuwa ana pakwa kwa mwili, na lazima pia nimpee dawa ya kula.  Nikimpea dawa hiyo alikuwa ananipiga juu alikuwa na hasira zingine alikuwa ana nitandika mbaya, lakini bado kila kitu namfanyia. Nikianzia kumuosha kutoka saa mbili, nitamalizia saa tisa, juu kazi yenye nitafanyishwa na huyo mama haikuwa rahisi. Tukimalizana ndiyo akubali nimpe dawa ndiyo akubali kulala, nilikuwa nachoka sana. Lakini nikajipea nguvu nikasema juu nilikuwa nimeenda kutafuta kazi, na hizi pesa mtu analipwa ni pesa mingi, wacha tuu nifanye.

Nilifanya mpaka nilipofika miezi sita. Mama wa huyo familia alikuwa mama mzuri sana, so nikajifikiria kenye naweza fanya ndiyo nitoke kwa hiyo familia, nikaambia mama, “mama yangu ame kufa, na ju mimi ni first born, hawezi zikwa kama mimi siko.”

So nikamwambia anipe ruhusa niende nikamzike halafu nitarudi. Yule mama akaniuliza “ni ukweli utarudi?” Nikamwambia “eeh.” Mama kwa uzuri wake alinipia ndege ya kwenda na kurudi. So ilibidii niseme mum yangu ame kufa although hajakufa, ni ile uwongo tuu nili danganyana ndiyo nijitoe kwa hiyo mtego. So mi nikarudi Kenya, venye nilirudi lakini hata sikurudi na huko kwa mahali nilikuwa, nikaenda kwetu Murang’a.

Nilipoenda Murang’a ukumbuke pale mwanzo nilikuwa nimepeleka mpaka huyo kijana wangu nyumbani kwetu Murang’a. So nilipoenda huko kwetu tukaa kaa, nika ambia wazazi wangu wacheni nirudi Mathare nijue kenye nitafanya. Mama yangu ali niruhusu nikarudi Mathare nika acha watoto wangu wawili huko nyumbani.

Niliporudi Mathare nika kaa kwa rafiki mwingine tulikuwa tunaishi nay eye kitambo ndiyo sasa nika rudia tuu ile kazi sasa, hata si ya kuuza manguo, juu sina do. Nikarudia tuu ile kazi a kujiuza, nikajiuza kidogo, kidogo, venye nilifikisha miezi tatu, nikapata pesa nikakomboa nyumba yangu.

Kukomboa nyuma yangu ndiyo nikajiita mukutano nikajiuliza sasa hii ni kazi gani Wambo huwanga unafanya? Yule mama aka nikujia tena, akaniambia Wambo si urudie ile kazi yako ya kuuza manguo? Nikamwambia enyewe wacha nirudi.

Tukaenda nay eye, nikurid ile kazi yangu ya kuuza manguo, nika endelea, nika uza manguo, ndiyo nikaendea sasa watoto wangu nyumbani. Venye niliwaendea sasa si unaona niko na nyumba nika anza kukaa na watoto wangu, nikawaingiza hapo shule na ile pesa yenye nilikuwa nafanyia ya kuuza manguo.

Nika kaa nikiuza manguo na bado niko na watoto wangu wawili. So unaona mzigo niliondolea mama yangu, hana hiyo mzigo mkubwa lakini bado nilikuwa nasaidia juu kuna wenye walikuwa secondary kwetu nyumbani.

Ndiyo kuna kijana mwingine huko mtaani alikuwa anasimama MP, anaitwa Kanyi, alikuja aka tuelezea kuna organization ina jiita HAART, sikuwa naijua. So tukaskia HAART ina hoji watu mahali Fulani si ndiyo tuka enda, tuka enda tuka hojia tukauilizwa maswali, wenye washawai enda Saudi mlipitia yapi na yapi. Halafu tukaitwa na Sophie,wakatuchukua ni kama wanaweza kutusaidia na ni ukweli. Venye tulienda huko kwao kwa ofisi, wakaanza kutuita mkutano huko tunaenda tunajiongea, tukaanza kusomeshwa huko, mpaka ule mzigo mtu alikuwa nao anaskia ni kama inakuja ikimwondoka kidogo, kidogo.

Ndiyo kwanza hata kuna siku walikuja waka tusomesha mambo ya Biashara, walitusaidia na hela, kutoka hiyo wakati mi ile kazi yangu nilikuwa nafanya ya kuuza manguo nikajipiga jeki tena nikaendelea vizuri, nikaona naendelea vizuri.

Hata kutoka hiyo wakati mimi sijawahi rudi ile kazi ya kitambo nilikuwa nafanya, hata mihadarati yenye nilikuwa natumia nikaacha kabisa na nika kuwa mtu mwingine msafi na nika kuwa mtu mwingine brand new. Na kusema haki na ukweli, hizo vitu zote za vituko zote niliacha. Na nikakuwa mama mwingine mzuri mwenye analea watoto wake, mwenye hata nikiwekelea chakula kwa meza tukikula tunaziombea juu najua mahali nimezitoa, nimezitoa mahali halali. Mahali najua hakuna kitu yoyote mbaya nimefanya, na nika anza kulea watoto wangu na kutoka hiyo wakati sija wahi ongezea mtoto mwingine, nikaambia Mungu anisaidie na hawa wawili ame nipa, wacha niwalee mpaka Mahali Mungu mwenyewe ataona nina faa. Siku ile Mungu atanipea bwana mwingine nitaolewa naweza taka kuolewa am ahata kama sita olewa, ile kazi nafanya Mungu aiisaidie kabisa iendelee niweze kulea hawa watoto wangu.

Kwa sahii tuna ongea nime jaribu na Mungu amenisaidia juu sahii mtoto wangu first born ako form 3 na huyo mwingine ako class 6 na naona bado naendelea vizuri.

Na kwa hayo nime ongea najua kuna wengine washapitia makubwa hata kuliko hata haya yangu yenye nimetaja. Na kuna mahali nimesahau kusema, mimi nikianza mambo ya wanaume, nilianza kitambo sana nilikuwa na miaka 12, kumi na mbili. Nikienda kuzaa ule mtoto wangu nilikuwa na miaka 15. Tebu anaglia hiyo distance, anaglia miaka yenye nilizaa nayo, angalia miaka yenye nilikuwa nayo nay ale makubwa nilikuwa napitia.

Huyu mtoto mdogo hivi alikuwa anajua kuvuta bangi, alikuwa anajua kutumia dawa, alikuwa anakunywa mpaka hizi chang’aa zenye anauza, na sa hizi ni mimi hapa, natoa ushuhuda ya kusema kuna Mungu wa siku ingine.

Juu kusema ukweli ni mimi ninaongea, ni mimi nimepitia hayo yote, na nimeshukuru sana kwa kunipea hiyo wakati, nimejiongea na naskia venye nimeongea ni kama nimepona, juu hii kidonda nimekaa nayo kwa miaka mingi na sija wahi iitoa. Na nimejitoa juu labda kuna mtu mwingine ashawahi pitia kama hayo nimepitia na kuna mwingine labda anaanza nimwambie aache, juu hakuna uzuri inatoka hapo.

Nina bahati niko hai sahii, labda kuna wengine wa hiyo wakati walikufa. Na pia huyo rafiki yangu mwenye alinitoa nyumbani kusema ukweli hayuko, alikufa. Juu yeye aliingilia hiyo maneno na akaendelea kabisa, yeye akaanza kuendea dawa Nigeria alikuwa sasa yeye yake ni ya kujidunga ika fika mahali yeye ali aga aka tuacha.

Lakini mimi natoa ushuhuda ya kusema kuna Mungu na nimeshukuru sana kwa huyo wakati yenye mumenipea na Mungu awabariki. Na Mungu abariki HAART na aibariki kabisa, iweze kutoa watu wengine kama sisi wenye walikuwa wanapitia manguma na sahii wame ji simamisha na miguu zao. Ahsanteni, Mungu awabariki.